
Duka la rejareja
Sukari, unga, sabuni — mauzo mengi madogo, kila siku.
Maduka ya kila aina Tanzania yanarekodi mauzo yao hapa kila siku.
Si programu sita. Ni moja, inayojua duka lako lote.
Skani msimbo, gusa bidhaa, au itaje kwa sauti. Risiti inatoka papo hapo — kwa taslimu, M-Pesa au benki.
Jaribu bureKila unachouza kinatolewa kwenye stoo yenyewe. Weka kiwango chako, na unaonywa kabla bidhaa haijaisha.
Jaribu bureNani anadaiwa, kiasi gani, na tangu lini. Kumbusha kwa WhatsApp bila ugomvi, na kila malipo yanaandikwa.
Jaribu bureRipoti ya leo, wiki na mwezi — ikiondoa gharama na matumizi, ili ujue ulichobakiza kweli.
Jaribu bureKila mfanyakazi anaingia kwa namba yake ya siri, na anaona kile unachomruhusu tu. Faida inabaki yako.
Jaribu bureTengeneza ankara kwa sekunde, chapisha risiti, au tuma kwa WhatsApp na barua pepe moja kwa moja.
Jaribu bureDuka lako halifungi saa kumi na mbili, na programu haifungi pia. Kila mauzo ya jioni yanaingia kwenye hesabu ya siku.
Anza bureKompyuta dukani, simu mfukoni — ni akaunti moja, na hesabu moja.
WebIngiza bidhaa nyingi kwa Excel mara moja, soma ripoti kwenye skrini kubwa, na tumia skana ya msimbo kama ya supermarket.
Fungua kwenye web
Android · iPhoneAndroid na iPhone. Akaunti ile ile unayotumia kwenye kompyuta — mauzo ya simu yanaonekana kwenye kompyuta mara moja.
Hakuna kinachosimama. Unaendelea kuuza kama kawaida.
Mauzo, madeni na bidhaa vinahifadhiwa ndani ya simu yako, na vina alama ya saa.
Kila kitu kinapanda chenyewe, na alama inabadilika kuwa tiki mbili.
Umeme na mtandao havitabiriki, lakini duka lako haliwezi kusubiri. Programu hii inaendelea, na inakuonyesha kila rekodi imefika wapi.
Jaribu bure“Sukari kilo mbili na mafuta lita moja”
Taja unachouza kwa Kiswahili cha kawaida. Programu inaandika mauzo na bei zake, wewe unathibitisha tu.
Jaribu burePokea malipo kwa msimbo mmoja wa QR — M-Pesa, Tigo Pesa na Airtel moja kwa moja. Mteja akilipa kwa njia mbili, kila njia inahesabiwa peke yake kwenye ripoti yako.
Taslimu, simu, benki au deni — hesabu ya droo yako inalingana na ripoti.
Anza bureUmekwama? Tuandikie WhatsApp au tupigie. Tunakujibu kwa Kiswahili, tunakuonyesha hatua kwa hatua, na tunakusaidia kuingiza bidhaa zako za kwanza.

Kutoka genge la mtaani hadi duka la jumla — kila mmoja anaipanga kwa jinsi yake.

Sukari, unga, sabuni — mauzo mengi madogo, kila siku.

Uza mita 3 kwenye roll ya mita 100 — stoo inapungua mita 3.

Saruji kwa mfuko, nondo kwa kipande, bei ya jumla kwa fundi.

Bidhaa ndogo nyingi, na onyo kabla kila moja haijaisha.

Tarehe za kuisha muda zinakumbukwa kwa ajili yako.

Skani msimbo wa kila spea, na uone faida ya kila moja.
Kwa dakika moja, kwa barua pepe au Google. Siku 3 za kwanza ni bure.

Andika bidhaa zako, skani misimbo yake, au ingiza orodha nzima kwa Excel.


Siku 3 za kwanza ni bure. Baada ya hapo, chagua muda unaokufaa — kila mpango una kila kitu.
Lipa kwa M-Pesa, Tigo Pesa, Airtel Money au Lipa Namba. Kwenye iPhone, kupitia App Store.

Jisajili kama wakala kwa namba ya simu na PIN. Kila mfanyabiashara unayemleta akilipia, unapata kuanzia TSh 1,000 hadi 15,000 — na unaiona ikiingia.
Kuwa wakalaHujapata jibu? Tuandikie WhatsApp.
Jisajili, tengeneza biashara yako, na uanze kurekodi mauzo papo hapo. Siku 3 za kwanza ni bure.
Ndiyo. Rekodi mauzo, bidhaa na madeni bila intaneti — taarifa husawazishwa zenyewe mtandao unaporejea.
Ndiyo. Tumia kwenye kompyuta kupitia web, na kwenye simu za Android na iPhone. Ni akaunti moja.
Ndiyo. Tengeneza msimbo mmoja wa QR na upokee M-Pesa, Tigo Pesa na Airtel moja kwa moja.
Hapana, isipokuwa ukiwaruhusu. Kila mfanyakazi anaona kile tu ulichomruhusu, na unaweza kuficha faida na gharama kabisa.
Ndiyo. Taarifa za biashara yako ni zako pekee, na zimehifadhiwa salama.
Jisajili kwa dakika moja na urekodi mauzo yako ya kwanza leo. Siku 3 za kwanza ni bure.
Anza bure